Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri

Mhubiri 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Jina zuri ni bora kuliko manukato ya gharama, na siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.
2Ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu, kwa kuwa maombolezo huja kwa watu wote wakati wa mwisho wa uhai, kwa hiyo watu wanaoishi ni lazima waweke hili moyoni.
3Huzuni ni bora kuliko kicheko, kwa kuwa baada ya uso wa huzuni huja furaha ya moyo.
4Moyo wa mwenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya karamu.
5Ni bora kusikiliza maonyo ya mtu mwenye hekima kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6Kwa kuwa kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Huu pia ni mvuke.
7kweli jeuri humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, na rusha huharibu moyo.
8Ni heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo; na watu wenye uvumilivu ni bora kuliko wenye majivuno rohoni.
9Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
10Usiseme, “Kwa nini siku za zamani zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa kuwa sio kwa sababu ya hekima kwamba unauliza swali hili.
11Hekima ni njema kama vitu vya thamani tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu. Inatoa faida kwa wale wanaoliona jua.
12Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.
13Tafakaria matendo ya Mungu: Ni nani awezaye kuimarisha chochote alichokipindisha?
14Wakati nyakati vinakuwa njema, ishi kwa furaha katika hali hiyo, lakini wakati unapokuwa mbaya, tafakari hili: Mungu ameruhusu hali zote ziwepo, Kwa sababu hii, hakuna mwanadamu yeyote atakaye fahamu chochote kinacho kuja baada yake.
15Nimeona mambo mengi katika siku zangu za ubatili. Kuna watu wenye haki ambao wanaangamia licha ya kwamba wana haki, na kuna watu waovu wanaoishi maisha marefu licha ya kwamba ni waovu.
16Usiwe mwenye haki katika macho yako mwenyewe. Kwa nini kujiharibu mwenyewe?
17Usiwe mwovu sana au mpumbavu. Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
18Ni vyema kwamba ushike hekima hii, na kwamba usiache haki iende zake. Kwa kuwa mtu amchae Mungu atatimiza ahadi zake zote.

19Hekima ina nguvu ndani ya mwenye hekima, zaidi ya watawala kumi katika mji.
20Hakuna mtu mwenye haki juu ya nchi anayefanya mema na hatendi dhambi.
21Usisikilize kila neno linaongelewa, kwa sababu unaweza kusikia mtumishi wako anakulaani.
22Vivyo hivyo unafahamu mwenyewe ndani ya moyo wako umewalaani wengine mara kadhaa.
23Haya yote nimeyathibitisha kwa hekima. Nikasema, “nitakuwa mwenye hekima,” lakini zaidi ambavyo ningekuwa.
24Hekima i mbali na kina sana. Ni nani awezaye kuipata?
25Nikageuza moyo wangu kujifunza kuchunguza na kutafuta hekima na ufafanuzi wa ukweli, na kufahamu kwamba ubaya ni ujinga na kwamba upumbavu ni wazimu.
26Nikapata kufahamu kwamba uchungu kuliko kifo, ndivo alivyo mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego, na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo. Yeyote ampendezaye Mungu ataponyoka kutoka kwake, lakini mwenye dhambi atachukuliwa naye.
27“Tafakari kile nilichovumbua,” asema Mwalimu. “Nimekuwa nikiongeza uvumbuzi mmoja hadi mwingine ili kwamba nipate ufafanuzi wa ukweli.
28Hii ndiyo bado natafuta, lakini bado sijapata. Sikupata mwanamme mmoja mwenye haki miongoni mwa elfu, lakini sikupata mwanamke miongoni mwa wale wote.
29Nimegundua hili: kwamba Mungu alimuumba binadamu akiwa mnyoofu, lakini wametoka katika hali ya unyofu wakitafuta magumu mengi.