Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 19

Luka 19:8-32

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.'
9Yesu akamwambia, 'Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.
10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea.'
11Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.
12Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.
13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.'
14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.'
15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.
16Wa kwanza akaja, akasema, `Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi.'
17Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi.'
18Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.'
19Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.'
20Na mwingine akaja, akasema, `Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,
21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda.'
22Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.'
25Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi.'
26'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu.”
28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
30akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
31Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua?' Semeni, “Bwana anamhitaji.”
32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.

Read Luka 19Luka 19
Compare Luka 19:8-32Luka 19:8-32