Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 10

Luka 10:25-34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?”
26Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”
27Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.”
28Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.”
29Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, Akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu.
31Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
32Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.
33Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. alipomuona, alisukumwa kwa huruma.
34Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.

Read Luka 10Luka 10
Compare Luka 10:25-34Luka 10:25-34