Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 10:25-34 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 10:25-34 in Biblia Takatifu

25 Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?”
26 Yesu akamwuliza, “Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?”
27 Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
28 Yesu akawaambia, “Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi.”
29 Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyang'anya mali yake na kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu.
31 Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
32 Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali akamwona, akapita kando.
33 Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma.
34 Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai; na kuyafunga halafu akampandisha juu ya punda wake akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamuuguza.
Luka 10 in Biblia Takatifu

Luka 10:25-34 in Biblia ya Kiswahili

25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?”
26 Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”
27 Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.”
28 Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.”
29 Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, Akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu.
31 Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
32 Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.
33 Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. alipomuona, alisukumwa kwa huruma.
34 Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.
Luka 10 in Biblia ya Kiswahili