Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 6

Yoshua 6:21-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Waliteketeza kabisa kila kitu kilichokuwa katika mji kwa makali ya upanga - wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, ng'ombe, kondoo na punda.
22Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, “Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwapia.”
23Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.
24Na ndipo waliuteketeza mji na kila kitu ndani yake. Isipokuwa fedha, dhahabu na vyombo vya fedha na chuma viliwekwa kwa hazina ya nyumba ya Yahweh.
25Bali Yoshua alimruhusu Rahabu kahaba, nyumba ya baba yake, na wote waliokuwa pamoja naye waishi. Mpaka leo hivi anaishi Israeli kwasababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko.
26Kisha katika kipindi hicho, Yoshua aliwaamuru kwa kiapo na kusema, “Alaaniwe machoni pa Yahweh mtu yule anayeujenga mji huu, Yeriko. Ataujenga msingi kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza, na kwa gharama ya mzaliwa wake wa pili atapachika milango yake.”

Read Yoshua 6Yoshua 6
Compare Yoshua 6:21-26Yoshua 6:21-26