Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi

Waamuzi 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Malaika wa Bwana akatoka Gilgali, akaenda Bokimu, akasema, “Nimekuleta kutoka Misri, na nimekuleta katika nchi niliyoapa kuwapa baba zako.
2Nikasema, 'Sitakuvunja kamwe agano langu na wewe. Usifanye agano na wale wanaoishi katika nchi hii. Ziangushe madhabahu zao. Lakini hukusikiliza sauti yangu. Je! ni nini hiki ulichokifanya?
3Basi sasa nasema, “Sitawafukuza Wakanaani mbele yenu, nao watakuwa miiba kwenu, na miungu yao itakuwa mtego kwa ajili yenu.”
4Malaika wa Bwana alipowaambia maneno hayo kwa watu wote wa Israeli, watu wakapiga kelele na kulia.
5Waliita mahali hapo Bokimu. Hapo wakatoa dhabihu kwa Bwana.
6Yoshua alipowaruhusu watu waende zao, wana wa Israeli kila mmoja akaenda mahali alipopewa, wakiwa na umiliki wa ardhi yao.
7Watu walimtumikia Bwana wakati wa maisha ya Yoshua na wazee walioendelea baada yake, ni wale waliokuwa wameona matendo yote makuu ya Bwana aliyoyafanya kwa Israeli.
8Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, alikufa akiwa na umri wa miaka 110.
9Wakamzika ndani ya mpaka wa nchi aliyopewa huko Timnath Heresi, katika mlima wa Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaash.
10Kizazi hicho chote kilikusanyika kwa baba zao. Kizazi kingine kilichofuata baada yao ambao hakikumjua Bwana au kile alichokifanya kwa Israeli.
11Watu wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
12Wakaondoka kwa Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa kutoka Misri. Wakaifuata miungu mingine, miungu ya watu waliokuwa karibu nao, nao wakaisujudia. Wakamkasirisha BWANA kwa sababu
13waliondoka kwa Bwana na kumwabudu Baal na Maashtoreti.
14Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao. Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao.
15Israeli walipokwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda, kama alivyowaapia. Na walikuwa katika shida kali.
16Ndipo Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa katika mikono ya wale waliokuwa wakiba mali zao.
17Hata hivyo hawakuwasikiliza waamuzi wao. Hawakuwa waaminifu kwa Bwana na wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao-wale waliotii amri za Bwana-lakini wao wenyewe hawakufanya hivyo.
18Bwana aliinua waamuzi kwa ajili yao, Bwana akawasaidia waamuzi na kuwakomboa kutoka kwa mikono ya adui zao siku zote muamuzi aliishi. Bwana aliwahurumia walipougua kwa sababu ya wale waliowadhulumu na kuwasumbua.

19Lakini mwamuzi alipokufa, waligeuka na kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko baba zao walivyofanya. Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.
20Hasira ya Bwana iliwaka juu ya Israeli; akasema, Kwa sababu taifa hili limevunja masharti ya agano langu ambalo nililiweka kwa ajili ya baba zao-kwa sababu hawakuisikiliza sauti yangu.
21Tangu sasa sitaliondoa mbele yao taifa lolote aliloliacha Yoshua baada ya kufa.
22Nitafanya hivi ili kuwajaribu Israeli, ikiwa watafuata njia ya Bwana au sivyo, kama vile baba zao walivyoifuata.
23Ndiyo sababu Bwana aliwaacha mataifa hayo, wala hakuwafukuza haraka na kuwatia mikononi mwa Yoshua.