Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi

Waamuzi 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa Bwana aliyaacha mataifa haya yaijaribu Israeli, yaani kila mtu katika Israeli ambaye hakushiriki vita yoyote huko Kanaani.
2(Alifanya hivyo ili kuwafundisha vita kizazi kipya cha Waisraeli ambao hawakujua kabla).
3Haya ndio mataifa: wafalme watano kutoka kwa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, na Wahivi waliokaa milima ya Lebanoni, kutoka Mlima Baali Hermoni hadi Hamathi.
4Mataifa haya yaliachwa kama njia ambayo Bwana angeijaribu Israeli, kuthibitisha kama watazitii amri alizowapa babu zao kupitia Musa.
5Basi wana wa Israeli wakakaa kati ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Waperizi, na Wahivi, na Wayebusi.
6Waliwachukua binti zao kuwa wake zao, nao wakawapa wana wao binti zao, nao wakaitumikia miungu yao.
7Wana wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wakamsahau Bwana, Mungu wao. Waliabudu Baali na Asherah.
8Basi, hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawauza mkononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Aram Naharaimu. Watu wa Israeli walitumikia Kushan Rishathaimu kwa miaka nane.
9Watu wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamuinua mtu atakayewasaidia wana wa Israeli, na mtu atakayewaokoa: Othnieli mwana wa Kenazi (ndugu mdogo wa Kalebu).
10Roho wa Bwana akamtia nguvu, naye akahukumu Israeli na akatoka kwenda vitani. Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu. Mkono wa Othnieli alishinda Kushan Rishathaimu.
11Nchi ilikuwa na amani kwa miaka arobaini. Ndipo Otinieli mwana wa Kenazi akafa.
12Baada ya hayo, Waisraeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; Bwana akampa Egloni mfalme wa Moabu nguvu, kuwashinda Waisraeli.
13Eglon alijiunga na wana wa Amoni na Waamaleki wakaenda na kuwashinda Israeli, na walichukua mji wa Mitende.
14Watu wa Israeli walimtumikia Eglon mfalme wa Moabu kwa miaka kumi na nane.
15Wana wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamwinua mtu aliyewasaidia, Ehudi mwana wa Gera, Mbenjamini, mtu shoto. Wana wa Israeli wakamtuma kwa Egloni, mfalme wa Moabu, kwa malipo yao ya kodi.
16Ehudi akajifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wa dhiraa moja; aliufunga chini ya nguo zake juu ya mguu wake wa kulia.
17Akampa Egloni Mfalme wa Moabu malipo ya kodi. (Egloni alikuwa mtu mnene sana.)
18Baada ya Ehudi kulipa malipo ya kodi, aliondoka na wale waliokuwa wameibeba.

19Hata hivyo Ehudi mwenyewe, alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali, akageuka na kurudi, akasema, 'Nina ujumbe wa siri kwako, mfalme wangu.' Eglon akasema, 'Nyamazeni kimya!' Kwa hiyo wote waliomtumikia wakatoka kwenye chumba.
20Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake.
21Ehudi akanyoosha mkono wake wa kushoto na akachukua upanga kutoka mguu wake wa kulia, na akautia ndani ya mwili wa mfalme.
22Na kipini cha upanga kikaingia ndani yake baada ya upanga, nao ukatokea nyuma yake, na mafuta yakashikamana juu ya upanga, kwa kuwa Ehudi hakuutoa upanga nje ya mwili wake.
23Kisha Ehudi akatoka kwenye ukumbi na akafunga milango ya chumba cha juu nyuma yake na akawafungia.
24Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, 'Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.'
25Walizidi kuwa na wasiwasi hata walipoanza kuhisi kuwa walikuwa wakipuuza wajibu wao wakati mfalme bado hakufungua milango ya chumba cha juu. Kwa hiyo walichukua ufunguo wakawafungua, tazama bwana wao, ameanguka chini, amekufa.
26Wakati watumishi wakisubiri, wakijiuliza nini wanapaswa kufanya, Ehudi alikimbia na kupita mahali ambako kulikuwa na sanamu za kuchonga, na hivyo akakimbia kwenda Seira.
27Alipofika, alipiga tarumbeta katika nchi ya mlima wa Efraimu. Kisha wana wa Israeli wakashuka pamoja naye kutoka milimani, naye akawaongoza.
28Akawaambia, Nifuate, kwa kuwa Bwana atawashinda adui zenu, Wamoabu. Wakamfuata, wakakamata vivuko vya Bonde la Yordani, toka kwa Wamoabi, wala hawakuruhusu mtu yeyote kuvuka mto.
29Wakati huo waliwaua watu elfu kumi wa Moabu, na wote walikuwa watu wenye nguvu na wenye uwezo. Hakuna aliyekimbia.
30Kwa hiyo siku hiyo Moabu ilishindwa na nguvu ya Israeli. Na nchi ilikuwa na amani kwa miaka thelathini.
31Baada ya Ehudi, mwamuzi aliyefuata alikuwa Shamgari mwana wa Anathi ambaye aliwaua Wafilisti 600 kwa konzo la ng'ombe. Pia aliwaokoa Israeli kutoka kwenye hatari.