Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi

Waamuzi 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo watu wote wa Israeli wakatoka kama mtu mmoja, toka Dani mpaka Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi; nao wakakusanyika mbele za Bwana huko Mispa.
2Viongozi wa watu wote, wa kabila zote za Israeli, wakachukua nafasi zao kwenye kusanyiko la watu wa Mungu-watu 400, 000 waendao kwa miguu, ambao walikuwa tayari kupigana na upanga.
3Basi wana wa Benyamini waliposikia kwamba watu wa Israeli walikuwa wamepanda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, “Tuambieni ni kwa namna gani huu uovu umefanyika.”
4Mlawi, mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu, Nilikuja Gibea katika nchi ya Benyamini, mimi na suria wangu, ili tulale.
5Wakati wa usiku, viongozi wa Gibea walinishambulia, wakizunguka nyumba na wakakusudia kuniua. Walimkamata na kumbaka suria wangu, naye akafa.
6Nilimchukua suria wangu na kumkata mwili wake vipande vipande, na kuweka katika kila nchi ya urithi wa Israeli, kwa sababu wamefanya uovu huo na upumbavu katika Israeli.
7Sasa, ninyi Waisraeli wote, toeni maneno na ushauri wenu hapa.”
8Watu wote wakaondoka pamoja kama mtu mmoja, wakasema, Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake, wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake.
9Lakini sasa hivi ndivyo tutakavyoifanyia Gibea tutaishambulia kama kura inavyotuongoza.
10Tutachukua watu kumi katika mia moja katika makabila yote ya Israeli, na mia moja katika elfu, na elfu moja katika elfu kumi, kuwapa chakula kwa ajili ya watu hawa, ili waweze kufika Gibea katika Benyamini, watawaadhibu kwa uovu wao waliofanya katika Israeli.
11Basi askari wote wa Israeli wakakusanyika juu ya mji, kama mtu mmoja.
12Makabila ya Israeli waliwatuma watu kwa kabila lote la Benyamini, wakisema, “Uovu huu uliofanywa kati yenu ni nini?
13Kwa hiyo, tupeni watu hao waovu wa Gibea, tupate kuwaua, na hivyo tutaondoa kabisa uovu huu kutoka kwa Israeli.” Lakini Wabenyamini hawakusikiliza sauti ya ndugu zao, watu wa Israeli,
14Ndipo wana wa Benyamini wakakusanyika kutoka mijini kwenda Gibea, wakajiandaa kupigana na wana wa Israeli.
15Watu wa Benyamini wakakusanya kutoka miji yao ili kupigana siku ile, askari elfu ishirini na sita waliopangwa kupigana na upanga. Walakini, kuna watu mia saba waliochaguliwa kutoka kwa wenyeji wa Gibea.
16Miongoni mwa askari wote hawa walikuwa watu mia saba waliochaguliwa ambao walikuwa wenye shoto. Kila mmoja wao angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose.
17Watu wa Israeli, bila kuhesabu namba kutoka kwa Benyamini, walikuwa na watu 400, 000 waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga. Wote hawa walikuwa watu wa vita.
18Watu wa Israeli waliondoka, wakaenda Betheli, wakaomba ushauri kutoka kwa Mungu. Wakauliza, “Ni nani kwanza atakayewaangamiza watu wa Benyamini kwa ajili yetu?” Bwana akasema, “Yuda atashambulia kwanza.”

19Watu wa Israeli waliamka asubuhi na wakahamisha kambi yao karibu na Gibea.
20Watu wa Israeli walikwenda kupigana na Benyamini. Wakaweka nafasi zao za vita dhidi yao huko Gibea.
21Watu wa Benyamini wakatoka Gibea, nao wakawaua watu elfu ishirini na mbili wa jeshi la Israeli siku ile.
22Wana wa Israeli walijitia nguvu wenyewe, na wakaunda mstari wa vita mahali pale walipokwisha kuchukua nafasi siku ya kwanza.
23Na wana wa Israeli wakaenda, wakalia mbele za Bwana hata jioni. Walitaka mwongozo kutoka kwa Bwana “Je, tunapaswa kwenda tena kupigana na ndugu zetu, watu wa Benyamini?” Naye Bwana akasema, “Wapigeni!”
24Basi watu wa Israeli wakapigana na askari wa Benyamini siku ya pili.
25Siku ya pili, Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea, nao wakawaua watu wa Israeli elfu kumi na nane. Wote walikuwa watu ambao walijifunza kupigana na upanga.
26Basi askari wote wa Israeli na watu wote wakaenda Betheli, wakalia, wakakaa mbele za Bwana; nao wakafunga siku hiyo hata jioni, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
27Wana wa Israeli wakamwomba Bwana, - kwa sababu ya sanduku la agano la Mungu lilikuwapo siku hizo;
28na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, aliyekuwa akihudumia mbele ya sanduku siku hizo. “Je twende vitani tena dhidi ya watu wa Benyamini, ndugu zetu, au tuache?” Bwana akasema, “Wapigeni, kwa maana kesho nitawasaidia kuwashinda.
29Basi Israeli akaweka watu mahali pa siri karibu na Gibea.
30Watu wa Israeli wakapigana na wana wa Benyamini kwa siku ya tatu, nao wakajenga vita vyao juu ya Gibea, kama walivyotangulia.
31Watu wa Benyamini wakaenda kupigana na watu, nao wakachukuliwa mbali na mji. Walianza kuua baadhi ya watu. Kulikuwa na watu thelathini wa Israeli ambao walikufa katika mashamba na barabara. Njia moja ilienda Betheli, na nyingine ikaenda Gibea.
32Ndipo wana wa Benyamini wakasema, “Wameshindwa na wanatukimbia, kama hapo awali.” Lakini askari wa Israeli wakasema, “Hebu tukimbie na kuwavuta mbali na mji hadi barabarani.”
33Watu wote wa Israeli waliondoka kutoka mahali pao na wakajipanga kwa vita huko Baal-Tamari. Basi askari wa Israeli waliokuwa wakijificha mahali pa siri walikimbia kutoka Maare-Geba.
34Wakatoka juu ya Gibea watu kumi elfu waliochaguliwa kutoka Israeli yote, na vita vilikuwa kali, lakini Wabenjamini hawakujua kwamba msiba ulikuwa karibu nao.
35Bwana akamshinda Benyamini mbele ya Israeli. Siku hiyo, askari wa Israeli waliwauawa watu wa Benyamini 25, 100. Wote hawa waliokufa walikuwa wale waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga.
36Basi askari wa Benyamini waliona wameshindwa. Wana wa Israeli walikuwa wametoa ardhi kwa Benyamini, kwa kuwa walikuwa wakihesabu watu waliowaweka katika nafasi zilizofichwa nje ya Gibea.

37Ndipo watu waliokuwa wameficha wakainuka na haraka na wakamkimbia Gibea. Nao wakauawa kila mtu aliyeishi mjini kwa upanga wao.
38Ishara iliyopangwa kati ya askari wa Israeli na watu waliojificha kwa siri itakuwa wingu kubwa la moshi litatokea nje ya mji.
39Ishara ilipokuja askari wa Israeli wakageuka kutoka kwenye vita. Basi Benyamini wakaanza kushambulia na wakawaua watu wa Israeli thelathini, wakasema, “Hakika wanapigwa mbele yetu, kama katika vita vya kwanza.”
40Lakini wakati nguzo ya moshi ilipoanza kuinuka nje ya mji, Wabenjamini waligeuka na kuona moshi ukitanda mbinguni kutoka mji mzima.
41Ndipo watu wa Israeli wakawageuka. Wana wa Benyamini waliogopa, kwa sababu waliona kwamba maafa yaliwajia.
42Basi wakakimbia kutoka kwa wana wa Israeli, kuelekea njia ya jangwani. Lakini vita viliwapata. Askari wa Israeli walitoka mijini na wakawaua pale waliposimama.
43Waliwalzungukia wana wa Benjamini na wakawafuata. Nao wakawakanyaga huko Noha, wakawaua mpaka upande wa mashariki wa Gibea.
44Kutoka kabila la Benyamini, watu kumi na nane elfu walikufa, wote walikuwa wanaume waliojulikana katika vita.
45Wakageuka na kukimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Waisraeli waliuawa zaidi ya elfu tano kati yao barabarani. Waliendelea kuwafuata, wakifuata kwa njia kuu kwenda Gidomu, na huko waliuawa elfu mbili zaidi.
46Askari wote wa Benyamini walioshuka siku hiyo walikuwa watu ishirini na tano waliokuwa wamejifunza kupigana kwa upanga; wote walikuwa wanajulikana katika vita.
47Lakini watu mia sita wakageuka na kukimbilia jangwani, kuelekea mwamba wa Rimoni. Wakakaa katika mwamba wa Rimoni kwa muda wa miezi minne.
48Askari wa Israeli waliwarudia watu wa Benyamini na wakawashinda na kuwaua-mji mzima, ng'ombe, na kila kitu walichopata. Pia walichoma moto kila mji katika njia yao.