1Usijisifu kwa ajili ya kesho, maana hujui siku italeta nini.
2Mtu mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe, mgeni na wala si midomo yako mwenyewe.
3Fikiria uzito wa jiwe na uzito wa mchanga- uchokozi wa mpumbavu ni mzito zaidi kuliko hivyo vyote.
4Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
5Ni bora karipio la wazi kuliko upendo uliofichwa.
6Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
7Mtu aliyekula na kushiba hulikataa hata sega la asali, bali kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu ni kitamu.