Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 1

Mithali 1:26-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
26Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu-
27hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata.
28Halafu wataniita, nami sitawajibu; wataniita katika hali ya kukata tamaa lakini hawataniona.
29Kwa sababu wamechukia maarifa na hawakuchagua kuwa na hofu ya Yehova,
30hawakufuata mafundisho yangu na wakayadharau masahihisho yangu yote.
31Watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa kwa matunda ya hila zao wenyewe.
32kwa maana wajinga hufa wanaporudi nyuma, na kutojali kwa wapumbavu kutawaangamiza.
33Bali kila anisikilizaye ataishi kwa usalama na atapumzika salama pasipo hofu ya maafa.

Read Mithali 1Mithali 1
Compare Mithali 1:26-33Mithali 1:26-33