23Mtu mwovu hukubali rushwa ya siri ili kupotosha njia za haki.
24Mwenye ufahamu huelekeza uso wake kwenye hekima, bali macho ya mpumbavu huelekea ncha za dunia.
25Mwana mpumbavu ni huzuni kwa baba yake na uchungu kwa mwanamke aliyemzaa.
26Pia, si vizuri kumwadhibu mwenye kutenda haki; wala si vema kuwachapa mjeledi watu waadilifu wenye ukamilifu.
27Mwenye maarifa hutumia maneno machache na mwenye ufahamu ni mtulivu.
28Hata mpumbavu hudhaniwa kuwa na busara kama akikaa kimya; wakati anapokaa amefunga kinywa chake, anafikiriwa kuwa na akili.