1Anayependa mafundisho hupenda maarifa, bali yule anayechukia maonyo ni mpumbavu.
2Yehova humpa fadhila mtu mwema, bali mtu ambaye hufanya mipango ya ufisada atahukumiwa.
3Mtu hawezi kuimarishwa kwa uovu, bali wale watendao haki hawawezi kung'olewa.
4Mke mwema ni taji ya mume wake, bali yule aletaye aibu ni kama ugonjwa unaoozesha mifupa yake.
5Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu.
6Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
7Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.
8Mtu husifiwa kwa kadri ya hekima yake, bali yule anayechagua ukaidi hudharauliwa.
9Bora kuwa na cheo duni- kuwa mtumishi tu- kuliko kujisifu kuhusu ukuu wako bila kuwa na chakula.
10Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.
11Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.
12Watu waovu hutamani wanavyoiba watu wabaya kutoka kwa wengine, bali tunda la wale watendao haki hutoka kwao mwenyewe.