Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Joeli

Joeli 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Tazama, katika siku hizo na wakati huo, nitakaporudi mateka wa Yuda na Yerusalemu,
2Nami nitakusanya mataifa yote, na kuwaleta mpaka bonde la Yehoshafati. Nitawahukumu huko, kwa sababu ya watu wangu na warithi wangu Israeli, ambao waliwatawanya kati ya mataifa, na kwa sababu waligawanya nchi yangu.
3Wamepiga kura kwa ajili ya watu wangu, walinunua kijana kwa ajili ya kahaba, kuuza msichana kwa divai ili waweze kunywa.
4Sasa, kwa nini unanikasirikia, Tiro, Sidoni na mikoa yote ya Wafilisti? Je! mutanirudishia malipo? Hata kama mutanilipa, mara moja nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
5Kwa maana mumechukua fedha zangu na dhahabu zangu, nanyi mukachukua hazina zangu za thamani na kuzileta katika hekalu zenu.
6Mumewauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kuwaondoa mbali na maeneo yao.
7Tazama, nitawaamsha, watoke mahali ambako muliwauza, na nitawarudishia malipo juu ya vichwa vyenu wenyewe.
8Nitawauza wana wako na binti zako, kwa mkono wa watu wa Yuda. Wao watawauza Sheba, kwa taifa mbali. Kwa maana Bwana amesema.
9Tangaza hii kati ya mataifa, 'Jitayarisheni wenyewe kwa ajili ya vita, waamsheni mashujaa, waacheni wakaribie, mashujaa wote wa vita wapande juu.
10Yafueni majembe yenu kuwa panga na visu vyenu vya kuchongea kuwa mikuki. Basi wadhaifu waseme, 'Nina nguvu.'
11Haraka na mje, mataifa yote ya karibu, jikusanyeni pamoja huko. Ee Bwana, washushe mashujaa wako.
12Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitakaa huko kuhukumu mataifa yote ya jirani.
13Wekeni katiki mundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, muponde zabibu, kwa ajiri pipa la divai limejaa. Vipuri vilivyofurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana.
14Kuna mshtuko, mshtuko katika bonde la Hukumu. Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu.
15Jua na mwezi vinakuwa giza, nyota zimeacha kuangaza.
16Bwana ataunguruma kutoka Sayuni, na kuinua sauti yake kutoka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika, lakini Bwana atakuwa makao kwa ajili ya watu wake, na ngome kwa wana wa Israeli.
17Kwa hiyo mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, anayeishi Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Kisha Yerusalemu itakuwa takatifu, na hakuna jeshi litaklozunguka tena.
18Katika siku hiyo, milima itatayarisha divai nzuri, milima itatiririsha maziwa, miito yote ya Yuda itapita katikati ya maji, na chemchemi zitakuja kutoka nyumba ya Bwana na maji ya bonde la Shitimu.

19Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vurugu iliyofanyika kwa watu wa Yuda, kwa sababu walimwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
20Lakini Yuda utakua mwenyeji milele, na Yerusalemu itakuwa kizazi hata kizazi.
21Nitawalipizia damu yao, ambayo sijajilipizia kisasi, kwa maana Bwana anaishi Sayuni.