4Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu.
5Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu.
6Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki.
7Maana kinywa changu hunena uaminifu na midomo yangu huchukia uovu.
8Maneno ya kinywa changu yote ni haki; hakuna kilichogeuzwa wala kupotoshwa.
9Maneno yangu yote yamenyooka kwa yule mwenye kuelewa; maneno yangu ni haki kwa wale wanaotafuta maarifa.
10Chagua fundisho langu badala ya fedha na maarifa kuliko dhahabu safi.
11Maana mimi, hekima ni bora kuliko vito; hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na mimi.
12Mimi, hekima, naishi kwa utaratibu, na ninamiliki maarifa na busara.
13Hofu ya Mungu ni kuchukia uovu- nachukia majivuno na kiburi, njia ya uovu, na kauli iliyopotoka- hivyo ninavichukia.
14Ninaushauri mzuri na hekima sahihi; mimi ni busara; nguvu zipo kwangu.
15Kwa njia yangu wafalme hutawala- pia na waungwana, na wote ambao hutawala kwa haki.
16Kwa njia yangu wafalme hutawala na waungwana na wote wanaotawala kwa haki.
17Nawapenda wale wanaonipenda, na wale wanaonitafuta kwa bidii, wataniona.
18Kwangu kunautajiri na heshima, utajiri wa kudumu na haki.
19Tunda langu ni bora kuliko dhahabu, bora hata kuliko dhahabu safi.
20Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki,
21katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
22Yehova aliniumba tokea mwanzo- mwazoni mwa matendo yake ya nyakati za kale.
23Tokea enzi za kale niliwekwa katika nafasi- tokea kwanza, tokea mwanzo wa dunia.
24Kabla ya bahari, mimi nilizaliwa- kabla ya kuwepo chemchemi zenye maji tele.
25Kabla ya milima na vilima kuwekwa, mimi nilizaliwa.
26Nilizaliwa kabla ya Yehova hajaiumba dunia wala makonde, hata mavumbi ya kwanza katika dunia.
27Nilikuwepo alipoziimarisha mbingu, wakati alipochora mstari katika sura ya kilindi.
28Nilikuwepo alipoimarisha anga la juu na wakati wa kutengeneza kina cha chemchemi.