3Kando ya njia ya kuingilia mjini, karibu na milango ya mji, anaita kwa sauti.
4Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu.
5Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu.
6Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki.
7Maana kinywa changu hunena uaminifu na midomo yangu huchukia uovu.
8Maneno ya kinywa changu yote ni haki; hakuna kilichogeuzwa wala kupotoshwa.
9Maneno yangu yote yamenyooka kwa yule mwenye kuelewa; maneno yangu ni haki kwa wale wanaotafuta maarifa.
10Chagua fundisho langu badala ya fedha na maarifa kuliko dhahabu safi.
11Maana mimi, hekima ni bora kuliko vito; hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na mimi.