11Kizazi ambacho kinachomlaa baba yao na hakimbariki mama yao,
12kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
13Hicho ni kizazi- jinsi gani macho yao yanakiburi na kope zao zimeinuka juu! -
14kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
15Ruba anamabinti wawili, “Toa na Toa” wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, “Inatosha”:
16Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, “Inatosha.”
17Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.