2Watenda mema wanapoongezeka, watu wanafurahi, bali wakati mtu mwovu anapotawala, watu huugua.
3Mwenye kupenda hekima baba yake anafurahi, bali anayeshikamana na makahaba huuharibu utajiri wake.
4Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
5Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.