15Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
16Watu waovu wanapotawala, uovu huongezeka, bali wenye kutenda haki wataona anguko la watu waovu.
17Mwadibishe mwanao naye atakupa pumziko; ataleta furaha katika maisha yako.
18Pasipo na maono ya kinabii watu huenda bila utaratibu, bali mwenye kuitunza sheria amebarikiwa.
19Mtumwa hawezi kurekebishwa kwa maneno, maana ingawa anaelewa, hakuna mwitikio.
20Je unamwona mtu mwenye haraka katika maneno yake? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
21Mwenye kumdekeza mtumwa wake tangu ujana, mwisho wake itakuwa taabu.
22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi na bwana mwenye hasira sana hutenda dhambi nyingi.
23Kiburi cha mtu humshusha chini, bali mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima.
24Anayeshirikiana na mwizi huyachukia maisha yake mwenyewe; husikia laana na wala hasemi chochote.
25Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.
26Wengi huutafuta uso wa mtawala, bali kutoka kwa Yehova huja haki kwa ajili yake.