10Mfukuze mbali mwenye dhihaka, na ugomvi utaondoka, mashindano na matukano yatakoma.
11Anayependa moyo safi na mwenye maneno ya neema, atakuwa rafiki yake mfalme.
12Macho ya Yehova huyaangalia maarifa, bali huyapindua maneno ya wadanganyifu.
13Mtu mvivu husema, “Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia.”
14Kinywa cha malaya ni shimo lenye kina kirefu; hasira ya Yehova huchochewa dhidi ya yule anayetumbukia ndani yake.
15Upumbavu umefungwa katika moyo wa mtoto, lakini marudi ya fimbo huutoa.