8Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;
9zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako.
10Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi katika dhambi zao, kataa kuwafuata.
11Kama watasema, “haya tufuatae, tuvizie ili kufanya mauaji, tujifiche ili tuwashambulie watu wasio na hatia, pasipo sababu.