1Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
2Mithali hizi zinafundisha hekima na maarifa, kufundisha maneno ya busara,
3ili mpate maarifa kwa ajili ya kuishi kwa kutenda wema, haki na adili.
4Mithali hizi zinatoa hekima kwa wale ambao hawakufunzwa, na kuwapa vijana maarifa na hadhari.