8Rushwa ni kama jiwe la kiini macho kwa yule ambaye atoaye; yeye anayeiacha, hufanikiwa.
9Anayesamehe kosa hutafuta upendo, bali yeye anayerudia jambo huwatenganisha marafiki wa karibu.
10Karipio hupenya ndani ya mtu mwenye ufahamu kuliko mapigo mamia kwenda kwa mpumbavu.
11Mtu mbaya hutafuta uasi tu, hivyo mjumbe katiri atatumwa dhidi yake.
12Ni bora kukutana na dubu aliyeporwa watoto wake kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
13Mtu anaporudisha mabaya badala ya mema, mabaya hayatatoka katika nyumba yake.
14Mwanzo wa mafarakano ni kama mtu anayefungulia maji kila mahali, hivyo ondoka kwenye mabishano kabla ya kutokea.
15Yeye ambaye huwaachilia watu waovu au kuwalaumu wale wanaotenda haki - watu hawa wote ni chukizo kwa Yehova.