Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 12

Mithali 12:5-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu.
6Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
7Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.
8Mtu husifiwa kwa kadri ya hekima yake, bali yule anayechagua ukaidi hudharauliwa.
9Bora kuwa na cheo duni- kuwa mtumishi tu- kuliko kujisifu kuhusu ukuu wako bila kuwa na chakula.
10Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.
11Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.
12Watu waovu hutamani wanavyoiba watu wabaya kutoka kwa wengine, bali tunda la wale watendao haki hutoka kwao mwenyewe.
13Mtu mbaya hunaswa kwa maongezi yake mabaya, bali wale watendao haki hujinasua katika taabu.
14Mtu hushiba vitu vyema kutokana na tunda la maneno yake, kama vile kazi ya mikono yake inavyompa thawabu.
15Njia ya mpumbavu ni sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu wa hekima husikiliza ushauri.
16Mpumbavu huonyesha hasira yake papo hapo, bali asiyejali tusi ni mwenye busara.
17Asemaye ukweli huongea ilivyo haki, bali shahidi wa uongo huongea uongo.
18Maneno yake asemaye kwa pupa ni kama kurusha upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
19Midomo yenye kweli itadumu milele, bali ulimi wa uongo ni kwa kitambo kidogo tu.
20Kuna udanganyifu katika mioyo ya wale wanaopanga kutenda uovu, bali furaha hutoka kwa washauri wa amani.
21Hakuna ugonjwa utakaowajia wale watendao haki, bali watu waovu watajazwa matatizo.

Read Mithali 12Mithali 12
Compare Mithali 12:5-21Mithali 12:5-21