2Yehova humpa fadhila mtu mwema, bali mtu ambaye hufanya mipango ya ufisada atahukumiwa.
3Mtu hawezi kuimarishwa kwa uovu, bali wale watendao haki hawawezi kung'olewa.
4Mke mwema ni taji ya mume wake, bali yule aletaye aibu ni kama ugonjwa unaoozesha mifupa yake.
5Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu.
6Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
7Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.