Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 1

Luka 1:33-48

Help us?
Click on verse(s) to share them!
33Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
34Mariamu akamwambia malaika, hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote?
35Malaika akajibu na akamwambia, “Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu.
36Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.
37Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”
38Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako.” Kisha malaika akamwacha.
39Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea.
40Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti.
41Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
42Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
43Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu?
44Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha.
45Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”
46Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana,
47na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
48Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.

Read Luka 1Luka 1
Compare Luka 1:33-48Luka 1:33-48