Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Nehemia

Nehemia 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo huo watu wa Israeli walikusanyika, nao walikuwa wamefunga, nao walikuwa wamevaa magunia, nao wakaweka vumbi juu ya vichwa vyao.
2Wazao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Walisimama na kukiri dhambi zao wenyewe na matendo maovu ya baba zao.
3Walisimama mahali pao, na robo ya siku walisoma kutoka Kitabu cha Sheria ya Bwana Mungu wao. Na robo nyingine ya siku walikiri na kuinama mbele ya Bwana Mungu wao.
4Walawi, Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebaniya, Buni, Sherebia, Bani na Kenani, walisimama juu ya ngazi, wakamwita Bwana, Mungu wao kwa sauti kubwa.
5Ndipo Walawi, na Yeshua, na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethalia, wakasema, “Simameni, mkamsifu Bwana, Mungu wenu, milele na milele.” “Libarikiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.
6Wewe ni Bwana. Wewe peke yako. Wewe umefanya mbinguni, mbingu za juu, na malaika wote wa vita vita, na dunia na kila kitu kilicho juu yake, na bahari na vyote vilivyomo. Unawapa wote uzima, na majeshi ya malaika wanakusujudia.
7Wewe ndiwe Bwana, Mungu aliyemchagua Abramu, akamtoa kutoka Uri wa Wakaldayo, akamwita Ibrahimu.
8Uliona moyo wake ulikuwa mkamilifu mbele yako, nawe ukafanya pamoja naye agano la kuwapa wazao wake nchi ya Wakanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Perizi, na Myebusi, na Wagirgashi. Umeweka ahadi yako kwa sababu wewe ni mwenye haki.
9Uliona shida ya baba zetu Misri na ukasikia kilio chao kando ya bahari ya shamu.
10Wewe ulifanya ishara na maajabu juu ya Farao, na watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake, kwa maana ulijua kwamba Wamisri walifanya kwa kujivunia. Lakini ulijifanyia jina ambalo linasimama hadi siku leo.
11Ukagawanya bahari mbele yao, wakavuka katikati ya bahari juu ya nchi kavu; na ukawatupa wale waliowa ndani ya kina, kama jiwe ndani ya maji ya kina.
12Wewe uliwaongoza kwa nguzo ya wingu wakati wa mchana, na kwa nguzo ya moto wakati wa usiku, ili kuwamulikia njiani waweze kutembea katika nuru yake.
13Ulishuka juu ya Mlima Sinai ukazungumza nao kutoka mbinguni ukawapa amri za haki na sheria za kweli, amri nzuri na maagizo.
14Uliwajulisha sabato yako takatifu, ukawapa amri, maagizo, na sheria kupitia Musa mtumishi wako.
15Uliwapa chakula kutoka mbinguni kwa ajili ya njaa yao, na maji kutoka mwamba kwa kiu yao, ukawaambia waende kuimiliki nchi uliyowaapa kwa kiapo kuwapa.
16Lakini wao na baba zetu walifanya uasi, nao walikuwa wakaidi, wala hawakuzitii amri zako.
17Walikataa kusikiliza, na hawakufikiri juu ya maajabu uliyofanya kati yao, lakini wakawa wakaidi, na katika uasi wao waliweka kiongozi ili wairudie hali ya utumwa. Lakini wewe ni Mungu ambaye amejaa msamaha, mwenye rehema na huruma, si mwepesi wa hasira, na wingi katika upendo thabiti. Wewe haukuwaacha.
18Wala hukuwaacha hata walipokwisha kutoa ndama katika chuma kilichochomwa na kusema, “Huyu ndio Mungu wenu aliyekuleta kutoka Misri,” wakati walipopotoka sana.

19Wewe, kwa huruma yako, hukuwaacha katika jangwa. Nguzo ya wingu iliyowangoza njiani haikuwaacha wakati wa mchana, wala nguzo ya moto usiku iliwaangazia barabara ambayo walipaswa kutembea.
20Uliwapa Roho wako mzuri kuwafundisha, na mana yako haukuwanyima kinywani mwao, na ukawapa maji kwa kiu yao.
21Kwa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, na hawakukosa chochote. Nguo zao hazikuchakaa na miguu yao haikuvimba.
22Uliwapa falme na watu, na ukawapa ardhi katika kila kona ya mbali. Basi wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
23Uliwafanya watoto wao kuwa wengi kama nyota za mbinguni, na ukawaingiza katika nchi. Uliwaambia baba zao waingie na kumiliki.
24Basi watu wakaingia, wakaimiliki nchi, ukawashinda wenyeji wa nchi hiyo, Wakanaani. Ukawatia mikononi mwao, pamoja na wafalme wao na watu wa nchi, ili Israeli afanye nao kama walivyotaka.
25Wao waliteka miji yenye nguvu na nchi yenye ustawi, nao wakachukua nyumba zenye vitu vyote vyema, birika zilizochimbwa, mizabibu na miti ya mizeituni, na miti ya matunda mengi. Kwa hiyo walikula na wakashiba na wakatosheka, na wakafurahi kwa wema wako.
26Basi hawakukutii na wakawaasi. Walitupa sheria yako nyuma ya migongo yao. Waliwaua manabii wako waliowaonya wakurudie wewe, nao wakafanya ukatili mkubwa.
27Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa adui zao, aliyewatesa. Na wakati wa mateso yao, walikulilia na wewe uliwasikia kutoka mbinguni na mara nyingi ukawaokoa katika mikono ya adui zao, kwa sababu ya huruma zako nyingi.
28Lakini baada ya kupumzika, wakafanya mabaya tena mbele yako, nawe ukawaacha mikononi mwa adui zao, kwa hiyo adui zao wakatawala juu yao. Hata walipokurudia na kukulilia, ukasikia kutoka mbinguni, mara nyingi ukawaokoa kwa sababu ya huruma yako.
29Uliwaonya ili wapate kurudi kwenye sheria yako. Hata hivyo walifanya kiburi na hawakusikiliza amri zako. Walifanya dhambi dhidi ya amri zako ambazo humpa uzima mtu yeyote anayezitii. Hawakuzitii, hawakuzitenda na walikataa kuzisikiliza.
30Kwa miaka mingi ukachukiliana nao na kuwaonya kwa Roho wako kwa njia ya manabii wako. Hata hivyo hawakusikiliza. Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa watu wa jirani.
31Lakini kwa huruma zako kubwa hukuwakomesha kabisa, au kuwaacha, kwa maana wewe ni Mungu mwenye rehema na mwenye huruma.
32Basi, Mungu wetu, Mungu wetu mkuu, mwenye nguvu na mwenye kutisha, unayeweka agano lako na upendo wako, shida zote zilizotupata sisi, wafalme wetu, wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote tangu siku za wafalme wa Ashuru mpaka leo usizihesabu kuwa ni kidogo.
33Wewe ni mwenye haki katika yote yaliyotupata, kwa kuwa umetenda kwa uaminifu, na tumefanya uovu.
34Wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, na baba zetu hawakuishika sheria yako, wala hawakuzingatia amri zako au shuhuda zako ulizowashuhudia.
35Hata katika ufalme wao wenyewe, wakati walifurahia wema wako kwao, katika nchi kubwa na yenye mazao uliyoweka mbele yao, hawakukutumikia au kuacha njia zao mbaya.
36Sasa sisi ni watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu kufurahia matunda yake na zawadi zake nzuri, na tazama, sisi ni watumwa!

37Mavuno mazuri kutoka nchi yetu huenda kwa wafalme uliowaweka juu yetu kwa sababu ya dhambi zetu. Watawala juu ya miili yetu na juu ya mifugo kama wanavyopenda. Tuna shida kubwa.
38Kwa sababu ya yote haya, tunafanya agano thabiti kwa kuandika. Kwenye hati iliyofungwa ni majina ya wakuu wetu, Walawi, na makuhani.”