Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Nehemia

Nehemia 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia Ikawa, katika mwezi wa Kisleu, katika mwaka wa ishirini, nilikuwa katika mji mkuu wa Sushani,
2mmoja wa ndugu zangu, Hanani, alikuja pamoja na watu wengine kutoka Yuda, nami nikawauliza kuhusu Wayahudi waliopona, Wayahudi waliosalia waliokuwa huko, na kuhusu Yerusalemu.
3Wakaniambia, “Wale waliokuwa katika mkoa ule waliookoka katika kifungo wapo katika shida kubwa na aibu kwa sababu ukuta wa Yerusalemu umebomolewa na milango yake imeteketezwa kwa moto.”
4Na mara tu niliposikia maneno haya, nikakaa na kulia, na kwa siku niliendelea kuomboleza na kufunga na kuomba mbele ya Mungu wa mbinguni.
5Ndipo nikasema, “Wewe ndiwe Bwana, Mungu wa mbinguni, Mungu uliye mkuu na kushangaza, unayetimiza agano na upendo wa kudumu pamoja na wale wanaokupenda na kushika amri zake.
6Sikiliza maombi yangu na fungua macho yako, ili uisikie sala ya mtumishi wako kwamba sasa nasali mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watu wa Israeli watumishi wako. Mimi ninakiri dhambi za watu wa Israeli, ambazo tumefanya dhidi yako. Wote mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.
7Tumefanya uovu sana juu yako, na hatukuzingatia amri, sheria, na hukumu ambazo ulimwamuru mtumishi wako Musa.
8Tafadhali kumbuka neno ulilomuamuru mtumishi wako Musa, 'mkitenda pasipo uaminifu, nitawatawanya kati ya mataifa,
9lakini mkirudi kwangu na kufuata amri zangu na kuzifanya, ingawa watu wako walienea chini ya mbingu za mbali, Nami nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali pale nilipopachagua ili kulifanya jina langu.'
10Sasa wao ni watumishi wako na watu wako, ambao uliwaokoa kwa nguvu yako kubwa na kwa mkono wako wenye nguvu.
11Bwana, naomba, sikiliza sasa maombi ya watumishi wako na sala ya watumishi wako ambao hufurahia kuheshimu jina lako. Sasa unifanikishe mimi mtumishi wako leo, na unijalie rehema mbele ya mtu huyu.” Nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.