2Juu ya kilima kando ya barabara, kwenye njia panda, hekima anasimama.
3Kando ya njia ya kuingilia mjini, karibu na milango ya mji, anaita kwa sauti.
4Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu.
5Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu.
6Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki.