12Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
13akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
14Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
15Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,
19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
23Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
24Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
25Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.
26Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote.
27Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake?
28Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake?
29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu.
30Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa.
31Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake.
32Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe.