18Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu:
19njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
20Hii ni njia ya mzinzi- anakula na kufuta kinywa chake na kusema, “sijafanya ubaya wowote.”
21Chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka na vinne haiwezi kuvivumilia:
22mtumwa anapokuwa mfalme; mpumbavu anaposhiba vyakula;
23mwanamke anayechukiwa anapoolewa; kijakazi anapochukua nafasi ya mkuu wake.
24Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara:
25mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
26Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba.
27Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio.
28Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.
29Kuna vitu vitatu ambavyo ni fahari katika mwendo na vinne ambavyo ni fahari katika namna ya kutembea:
30simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama- wala hajiepushi na kitu chochote;
31jogoo anayetembea kwa mikogo; mbuzi; na mfalme ambaye askari wapo kando yake.