1Maneno ya Aguri mwana wa Yake - mausia: Mtu huyu alimwambia Ithieli, kwa Ithiel na Ukali:
2Hakika nipo kama mnyama kuliko mwanadamu na sina ufahamu wa wanadamu.
3Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya Mtakatifu.
4Je ni nani amekwenda juu mbinguni na kurudi chini? Je ni nani aliyekusanya upepo kwenye mikono yake? Je ni nani aliyekusanya maji kwenye kanzu? Je ni nani aliyeziimarisha ncha za dunia yote? Jina lake ni nani, na jina la mtoto wake ni nani? Hakika unajua!
5Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
6Usiyaongezee maneno haya, au atakukemea, na utathibitishwa kuwa mwongo.