4Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
5Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
6Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
7Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
8Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.