2Watenda mema wanapoongezeka, watu wanafurahi, bali wakati mtu mwovu anapotawala, watu huugua.
3Mwenye kupenda hekima baba yake anafurahi, bali anayeshikamana na makahaba huuharibu utajiri wake.
4Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
5Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
6Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
7Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
8Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.
9Mtu mwenye busara anapojadiliana na mpumbavu, hughadhabika na kucheka, hakutakuwa na utulivu.
10Mkatili humchukia mwenye ukamilifu na hutafuta maisha ya mwenye haki.
11Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
12Kama matawala atazinagatia uongo, maafisa wake wote watakuwa waovu.