4Usifanye kazi sana ili kupata mali; uwe na busara ya kutosha ili ujue wakati wa kuacha.
5Je utaruhusu macho yako yaangaze juu yake? Itaondoka, maana itawaa mabawa kama tai na kuruka angani.
6Usile chakula cha yule mwenye jicho baya- na usiwe na shauku ya vinono vyake,
7maana ni mtu mwenye kuhesabu gharama ya chakula. “Kula na kunywa!” anakuambia, lakini moyo wake haupo pamoja nawe.
8Utatapika kiasi kidogo ulichokula na utakuwa umepoteza sifa zako njema.
9Usiongee katika usikivu wa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako.
10Usihamishe jiwe la mpaka wa kale au kunyang'anya mashamba ya yatima,
11maana Mkombozi wao ni imara na atatetea kesi yao dhidi yako.
12Elekeza moyo wako katika mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.
13Usizuie kuadilisha mtoto, maana ukimchapa kwa fimbo, hatakufa.
14Ni wewe unayepaswa kumchapa kwa fimbo na kuikoa nafsi yake kuzimu.
15Mwanangu, kama moyo wako una busara, basi moyo wangu utafurahi pia;
16sehemu zangu ndani kabisa zitafurahi sana midomo yako inaponena haki.
17Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote.