4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
5Makusudi ndani ya moyo wa mtu ni kama maji yenye kina, bali mtu mwenye ufahamu huyateka.
6Mara nyingi mtu husema yeye ni mwaminifu, lakini ni nani awezaye kumpata yule mwaminifu?
7Mtu atendaye haki hutembea katika uaminifu wake na wana wake wanaofuata baada yake wanafuraha.