4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
5Makusudi ndani ya moyo wa mtu ni kama maji yenye kina, bali mtu mwenye ufahamu huyateka.
6Mara nyingi mtu husema yeye ni mwaminifu, lakini ni nani awezaye kumpata yule mwaminifu?
7Mtu atendaye haki hutembea katika uaminifu wake na wana wake wanaofuata baada yake wanafuraha.
8Mfalme anayeketi kwenye kiti cha hukumu akifanya kazi za kuhukumu hupembua kwa macho yake mabaya yote yaliyoko mbele yake.
9Nani anayeweza kusema, “Nimeuweka safi moyo wangu; nipo huru na dhambi zangu”?
10Mizani tofauti na vipimo visivyosawa - Yehova huvichukia vyote.
11Hata kijana hujulikana kwa matendo yake, kwa mwenendo wake kama ni safi na uadilifu.
12Masikio yanayosikia na macho yanayoona- Yehova aliyafanya yote.