22“Mpaka lini enyi wajinga mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini enyi wenye dhihaka mtapenda dhihaka, na hadi lini enyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
23Zingatia karipio langu; nitatoa mawazo yangu kwa ajili yenu; nitawafahamisha maneno yangu.
24Nimeita, nanyi mkakataa kusikiliza; nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyezingatia.
25Lakini mumedharau mafundisho yangu yote na wala hamkuzingatia maelekezo yangu.
26Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu-
27hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata.
28Halafu wataniita, nami sitawajibu; wataniita katika hali ya kukata tamaa lakini hawataniona.