Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 1

Mithali 1:2-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Mithali hizi zinafundisha hekima na maarifa, kufundisha maneno ya busara,
3ili mpate maarifa kwa ajili ya kuishi kwa kutenda wema, haki na adili.
4Mithali hizi zinatoa hekima kwa wale ambao hawakufunzwa, na kuwapa vijana maarifa na hadhari.
5Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao na watu wenye ufahamu wapate mwongozo,
6kwa kuelewa mithali, misemo, vitendawili na maneno ya wenye busara.
7Hofu ya Yehova ni chanzo cha maarifa- wapumbavu hudharau hekima na nidhamu.
8Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;
9zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako.
10Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi katika dhambi zao, kataa kuwafuata.
11Kama watasema, “haya tufuatae, tuvizie ili kufanya mauaji, tujifiche ili tuwashambulie watu wasio na hatia, pasipo sababu.
12Haya tuwameza wakiwa hai, kama kuzimu inavyowachukua wenye afya, na kuwa kama wale waangukao kwenye shimoni.
13Tutapata vitu vyote vya thamani; tutazijaza nyumba zetu vile tunavyoiba kwa wengine.
14Weka vitu vyako kwetu; tutakuwa na mfuko moja kwa pamoja.”
15Mwanangu, usitembee katika njia moja pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa katika mapito yao;
16miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu.
17Kwa kuwa haina maana kumtegea ndege mtego wakati ndege anaona.

Read Mithali 1Mithali 1
Compare Mithali 1:2-17Mithali 1:2-17