15Mwanangu, usitembee katika njia moja pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa katika mapito yao;
16miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu.
17Kwa kuwa haina maana kumtegea ndege mtego wakati ndege anaona.
18Watu hawa huvizia kujiua wenyewe—wanatega mtego kwa ajili yao wenyewe.