Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 16

Mithali 16:13-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Mfalme hufurahia midomo ambayo husema haki na anampenda mwenye kusema waziwazi.
14Hasira ya mfalme ni mjumbe wa mauti lakini mtu mwenye busara atajaribu kutuliza hasira yake.
15Katika nuru ya uso wa mfalme ni uzima na fadhila yake ni kama wingu linaloleta mvua ya masika.
16Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu. Kuchagua kupata ufahamu ni zaidi kuliko fedha.
17Njia kuu ya watu waadilifu hujitenga na ubaya; mwenye kuyahifadhi maisha yake huilinda njia yake.
18Kiburi hutangulia kabla ya uharibifu na moyo wa kujivuna kabla ya maangamizi.
19Ni bora kunyenyekea miongoni mwa watu masikini kuliko kugawana ngawira pamoja watu wenye kiburi.
20Mwenye kutafakari yaliyofundishwa hupata kilicho chema na wenye kumtumaini Yehova watafurahi.
21Mwenye hekima moyoni anaitwa ufuhamu na utamu wa hotuba huongeza uwezo wa kufundisha.
22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake ambaye nayo, bali adhabu ya wapumbavu ni upumbavu wao.
23Moyo wa mtu mwenye hekima hutoa busara katika kinywa chake na huongeza ushawishi katika midomo yake.
24Maneno yenye kufaa ni sega la asali -matamu kwenye nafsi na huponya mifupa.

Read Mithali 16Mithali 16
Compare Mithali 16:13-24Mithali 16:13-24