7Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
8Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake.
9Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki.
10Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa.
11Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu?
12Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima.
13Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.
14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi.
15Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima.
16Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia.