21Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
22Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
23Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
24Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu.
25Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
26Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
27Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
28Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.