17Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
18Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.
19Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
20Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
21Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
22Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
23Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
24Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu.
25Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
26Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
27Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
28Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
29Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
30Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
31Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.