14Yule asiyemwaminifu atapata anachostahili kwa njia zake, bali mtu mwema atapata kilicho chake.
15Yeye ambaye hakufundishwa huamini kila kitu, bali mtu mwenye hekima huzifikiria hatua zake.
16Mtu mwenye hekima huogopa na kutoka kwenye ubaya, bali mpumbavu huliacha onyo kwa ujasiri.
17Yeye ambaye anakuwa na hasira kwa haraka hufanya mambo ya kipumbavu, na mtu anayefanya hila mbaya huchukiwa.
18Wajinga hurithi upumbavu, lakini watu wenye hekima wamezingirwa kwa maarifa.
19Hao ambao ni waovu watainama mbele yao walio wema na wale wenye uovu watasujudu kwenye malango ya wenye haki.