Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 11

Mithali 11:14-31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Pasipokuwa na uongozi wenye busara, taifa huanguka, bali ushindi huja kwa kushauriana washauri wengi.
15Anayemdhamini mkopo wa mgeni ataumia kwa usumbufu, bali anayechukia kutoa rehani kwa namna ya ahadi yupo salama.
16Mwanamke mwenye rehema hupata heshima, bali watu wakorofi hufumbata utajiri.
17Mtu mkarimu hufaidika mwenyewe, bali mkatili hujiumiza mwenyewe.
18Mtu mwovu husema uongo kupata mishahara yake, bali yeye apandaye haki anavuna mishahara ya kweli.
19Mtu mwaminifu atendaye haki ataishi, bali yeye atendaye uovu atakufa.
20Yehova anawachukia wenye ukaidi mioyoni, bali anawapenda wale ambao njia zao hazina makosa.
21Uwe na uhakika juu ya hili- watu waovu hawatakosa adhabu, bali uzao wa wale watendao haki watawekwa salama.
22Kama pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe ndiyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.
23Shauku ya wale watendao haki ni matokeo mema, bali watu waovu wanaweza kutumainia ghadhabu tu.
24Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini.
25Mtu mkarimu atafanikiwa na yule awapaye maji wengine atapata maji yake mwenyewe.
26Watu wanamlaani mtu ambaye hukataa kuuza nafaka, bali zawadi njema hufunika kichwa chake ambaye huuza nafaka.
27Yule ambaye hutafuta mema kwa bidii pia anatafuta kibali, bali yule atafutaye ubaya atapata ubaya.
28Wale wanaotumaini utajiri wataanguka, bali kama jani, wale watendao haki watasitawi.
29Yule ambaye analeta taabu kwenye kaya yake ataurithi upepo na mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye moyo wa hekima.
30Wale watendao haki watakuwa kama mti wa uzima, lakini vurugu huondoa uzima.
31Tazama! Ikiwa wale watendao haki hupokea wanachositahili, je si zaidi kwa waovu na wenye dhambi!

Read Mithali 11Mithali 11
Compare Mithali 11:14-31Mithali 11:14-31