Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 11

Mithali 11:1-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri.
2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima.
3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza.
4Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti.
5Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao.
6Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao.
7Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu.
8Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu.
9Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama.
10Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha.
11Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa.
12Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.
13Anayekwenda akizunguka kwa kukashifu hufunua siri, bali mtu mwaminifu hustiri jambo.
14Pasipokuwa na uongozi wenye busara, taifa huanguka, bali ushindi huja kwa kushauriana washauri wengi.

Read Mithali 11Mithali 11
Compare Mithali 11:1-14Mithali 11:1-14