Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 28

Matendo ya Mitume 28:20-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki.
21Kisha wakamwambia, “Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote baya kuhusu wewe.
22Lakini tunataka kusikia kutoka kwako unafikiri nini kuhusu hili kundi la watu hawa, kwa sababu inajulikana kwetu kwamba linaongea kinyume kila mahali.”
23Walipokuwa wametenga siku kwa ajili yake, watu wengi zaidi walimwijia mahali alipokuwa anaishi. Alisema lile jambo kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Mungu. Alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote mbili kutoka katika sheria za Musa na kutoka kwa manabii, kuanzia asubuhi hadi jioni.
24Baadhi yao walishawishika kuhusu mambo yale yaliyosemwa, wakati wengine hawakuamini.
25Waliposhindwa kukubaliana wao kwa wao, waliondoka baada ya Paulo kulisema jambo hili moja, “Roho Mtakatifu alisema vyema kupitia Isaya nabii kwa baba zenu.
26Alisema, 'Nenda kwa watu hawa useme, “Kwa masikio yenu mtasikia, lakini hamtaelewa; Na kwa macho yenu mtaona lakini hamtatambua.

Read Matendo ya Mitume 28Matendo ya Mitume 28
Compare Matendo ya Mitume 28:20-26Matendo ya Mitume 28:20-26