1Mitume na ndugu wale waliokuwa huko Yudea walisikia kuwa wamataifa wamelipokea neno la Mungu.
2Petro alipokuja huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa, Wakisema,
3“Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!”
4Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema,
5“Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu.
6Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani.
7Kisha nikasikia sauti ikisema nami, “Amka, Petro, chinja naj ule!”
8Nikasema, “Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu”
9Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi,
10Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.
11Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu.
12Roho akaniambia kwenda nao, na nisitofautiane nao. Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu mmoja.
13Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, “Nitume Yafa nikamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro.
14Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote.”
15Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni.
16Nakumbuka maneno ya Bwana, alivyosema, “Yohana alibatiza kwa maji; lakini mtabatizwa katika Roho mtakatifu.”
17Pia kama Mungu ametoa zawadi kama alizotupa sisi tulipoamini katika Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani, kwamba naweza kumpinga Mungu?
18Waliposikia mambo haya, hawakurudisha, bali walimsifu Mungu na kusema, “Mungu ametoa toba kwa ajili ya wa mataifa pia”
19Basi waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali, hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia. Waliwaambia ujumbe kuhusu Yesu peke yake kwa wayahudi na si kwa mwingine awaye yote.
20Lakini baadhi yao ni watu kutoka Kipro na Krene, walikuja Antiokia na kusema na wayunani na kumhubiri Bwana Yesu.
21Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na watu wengi waliamini na kumgeukia Bwana.
22Habari zao zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalem: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia.
23Alipokuja na kuona karama ya Mungu alifurahi; na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika mioyo yao.
24Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana.
25Baadaye Barnaba alienda Tarso kumwona Sauli.
26Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia.
27Na katika siku hizi manabii wakashuka kutoka Yerusalemu mpaka Antiokia.
28Mmoja wao ni Agabo ndilo jina lake, akasimama akiashiriwa na Roho kuwa njaa kali itatokea ulimwenguni mwote. Hii ilitokea wakati wa siku za Klaudio.
29Kwa hiyo, wanafunzi, kila mmoja alivyo fanikiwa, waliamua kupeleka misaada kwa ndugu walioko Uyahudi.
30Walifanya hivi; Walituma pesa kwa mkono wa Barnaba na Sauli.