Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume

Matendo ya Mitume 14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikatokea ndani ya Ikonio kwamba Paulo na Barnaba waliingia pamoja ndani ya sinagogi la Wayahudi nakuongea namna ambayo kundi kubwa la watu Wayahudi na Wayunani waliamini.
2Lakini wayahudi wasiotii waliwachochea akili wamataifa na kuwafanya kuwa wabaya dhidi ya ndugu.
3Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku akitoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya hivi kwa kutoa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba.
4Lakini eneo kubwa la mji liligawanyika: baadhi ya watu walikuwa pamoja na Wayahudi, na baadhi pamoja na mitume.
5Wakati wamataifa na Wayahudi walipojaribu kuwashawishi viongozi wao kuwatendea vibaya na kuwaponda mawe Paulo na Barnaba,
6wakalitambua hilo na kukimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale,
7na huko waliihubiri injili.
8Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hajawahi kutembea.
9Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa.
10Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, “Simama kwa miguu yako.” Na yule mtu aliruka juu na kuanza kutembea.
11Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, “miungu imetushukia kwa namna ya binadamu.”
12Walimwita Barnaba “Zeu,” na Paulo “Herme” kwa sababu alikuwa msemaji mkuu.
13Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka.
14Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka walikwenda nje kwenye umati, wakilia
15na kusema, “Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama za kwenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo.
16Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe.
17Lakini bado, hakuondoka pasipo shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha”
18Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka.

19Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa.
20Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, wakaingia mjini. Siku ya pili, aliende Derbe na Barnaba.
21Baada ya kufundisha injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikoniamu, na hadi Antiokia.
22Waliendelea kuimarisha nafsi za wanafunzi na kutiwa moyo kuendelea katika imani, akasema, “Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia mateso mengi.”
23Walipo wateua kwa ajili yao wazee wa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini.
24Kisha walipita katika Pisidia, walifika Pamfilia.
25Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia.
26Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha.
27Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kusanyiko la pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa.
28Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.