Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume

Matendo ya Mitume 19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko.
2Paulo akawaambia, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakamwambia, “Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu.”
3Paul alisema, “Sasa ninyi mlibatizwaje?” Wakasema, “Katika ubatizo wa Yohana.
4Basi Paulo akajibu, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu.”
5Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri.
7Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili.
8Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwavuta watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu.
9Lakini Wayahudi wengine walikuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea kila siku katika ukumbi wa Tirano.
10Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani.
11Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo,
12kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua leso na nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo.
13Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, “Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
14Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa.
15Roho wachafu wakawajibu, “Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani?
16“Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.
17Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.
18Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya.

19Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.
20Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika nguvu.
21ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso, Roho akamwongoza kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, “Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia.”
22Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda.
23Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia.
24Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi.
25Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, “Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi.
26Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba hakuna miungu ambayo imefanywa kwa mikono.
27Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu.”
28Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, “Diana wa Waefeso ni mkuu.”
29Mji wote ukajaa ghasia, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia.
30Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia.
31Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo.
32Baadhi ya watu walikuwa wakisema kitu hiki na wengine jambo lile, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja.
33Wayahudi wakamleta Iskanda nje ya umati wa watu na kumuweka juu mbele ya watu. Iskanda akatoa ishara kwa mkono wake kutoa maelezo kwa watu.
34Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, “Diana ni mkuu wa Wafeso.”
35Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, 'Enyi wanaume wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Diana mkuu na ile picha ilivyoanguka kutoka mbinguni?
36Kuona Basi kwamba mambo haya hayatawezekana, tunapaswa kuwa na utulivu na msifanye chochote kwa haraka.

37Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu mke.
38Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri.
39Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali.
40Kwa kweli tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza.
41Baada ya kusema haya, aliwatawanya makutano.